MASHARTI & VIGEZO

TERMS & CONDITIONS

Masharti & VigezoTerms & Conditions

Ilisasishwa mara ya mwisho: Novemba 2026

Last updated: November 2026

Tafadhali soma masharti haya kabla ya kuomba huduma zetu.

Please read these terms before requesting our services.

1. Kuhusu Masharti Haya1. About These Terms

Kwa kutumia tovuti hii au kuomba huduma kutoka DamyGaso Tech Solutions Limited ("sisi", "kampuni"), unakubaliana na masharti yafuatayo. Kwa miradi mikubwa au mikataba rasmi, makubaliano ya maandishi yatakayosainiwa yatatangulia pale yanapotofautiana na masharti haya.

By using this website or requesting services from DamyGaso Tech Solutions Limited ("we", "the company"), you agree to the following terms. For larger projects or formal contracts, the signed written agreement prevails wherever it differs from these terms.

2. Huduma Zetu2. Our Services

Tunatoa: IT, Network & Cybersecurity; Website, App & Software; Graphics, Branding & Printing; Logistics & Distribution (ikiwemo kupitia madukapoa); na Wi-Fi ya kibiashara (hotspot). Maelezo ya kila huduma yapo kwenye ukurasa wa Huduma.

We provide: IT, Network & Cybersecurity; Website, App & Software; Graphics, Branding & Printing; Logistics & Distribution (including through madukapoa); and commercial Wi-Fi (hotspot). Details of each service are on the Services page.

3. Bei na Quote3. Pricing & Quotes

Bei zilizo kwenye ukurasa wa Bei ni za kianzio na zinaweza kubadilika kulingana na ukubwa na utata wa kazi. Huduma zinazoandikwa "Omba Quote" hupewa quote maalum. Bei ya mwisho ni ile iliyokubaliwa kwenye quote au mkataba.

Prices on the Pricing page are starting prices and may vary with the size and complexity of the work. Services marked "Request a Quote" are quoted individually. The final price is the one agreed in the quote or contract.

4. Malipo4. Payment

Isipokuwa kama imekubaliwa vinginevyo kwa maandishi, miradi inahitaji malipo ya awali ya asilimia 30 kabla ya kazi kuanza, asilimia 40 baada ya kazi kukamilika na asilimia 30 wakati wa kukabidhi kazi ya mwisho.

Unless otherwise agreed in writing, projects require a 50% upfront deposit before work begins, with the remaining 50% due before final delivery.

5. Muda wa Kukamilisha Mradi5. Project Timelines

Muda wa kukamilisha hutegemea aina na ukubwa wa mradi, na utaelezwa wazi kabla ya kuanza kazi. Ucheleweshaji wa mteja kutoa maudhui, maamuzi au malipo unaweza kuathiri ratiba iliyopangwa.

Timelines depend on project type and scope and will be stated before work begins. Delays by the client in providing content, decisions or payment may affect the agreed schedule.

6. Marekebisho (Revisions)6. Revisions

Kila mradi unajumuisha idadi ya marekebisho iliyokubaliwa kwenye quote. Marekebisho ya ziada yanaweza kuwa na gharama ya ziada.

Each project includes the number of revisions agreed in the quote. Extra revisions may carry an additional cost.

7. Hosting, Domain na Matengenezo7. Hosting, Domain & Maintenance

Miradi ya website inayostahili inajumuisha mwaka 1 wa hosting, domain na business email bila malipo, pamoja na mwaka 1 wa matengenezo baada ya kukabidhi. Baada ya kipindi hicho, ada za uhuishaji wa kila mwaka zinatumika kama zilivyoainishwa kwenye ukurasa wa Bei. Mifumo mikubwa yenye VPS au database maalum hupangiwa bei ya uhuishaji kando.

Eligible website projects include one year of free hosting, domain and business email, plus one year of maintenance after handover. After that, annual renewal fees apply as listed on the Pricing page. Larger systems with a dedicated VPS or database are quoted separately for renewals.

8. IT Support na Urejeshaji wa Data8. IT Support & Data Recovery

Mteja anawajibika kuhifadhi nakala (backup) za data zake. Mafanikio ya urejeshaji wa data hutegemea hali ya kifaa, kwa hiyo hatuwezi kuhakikisha kurejesha data yote. Tutakueleza kwa uwazi hali ya kifaa na uwezekano wa kufanikiwa kabla ya kuanza kazi, na tutashughulikia data yako kwa usiri kama ilivyoelezwa kwenye Sera ya Faragha.

The client is responsible for keeping backups of their data. The success of data recovery depends on the condition of the device, so we cannot guarantee that all data will be recovered. We will explain the device's condition and the likelihood of success before starting, and we handle your data in confidence as described in the Privacy Policy.

9. Logistics na Wi-Fi ya Kibiashara9. Logistics & Commercial Wi-Fi

Masharti ya Logistics & Distribution (aina ya mzigo, uzito, umbali, njia na bima) yanaelezwa kwenye quote ya kila ombi. Huduma ya Wi-Fi ya kibiashara hufanyika kwa makubaliano ya maandishi kwa kila eneo, ikiwemo ugavi wa mapato na majukumu ya mmiliki wa eneo. Majukwaa kama madukapoa yanaweza kuwa na masharti yake ya matumizi.

Terms for Logistics & Distribution (cargo type, weight, distance, route and insurance) are set out in each request's quote. The commercial Wi-Fi service is provided under a written agreement per location, including revenue sharing and the location owner's responsibilities. Platforms such as madukapoa may have their own terms of use.

10. Haki Miliki10. Intellectual Property

Umiliki wa kazi ya mwisho (design, tovuti au maudhui) unahamishiwa kwa mteja baada ya malipo kamili. DamyGaso Tech Solutions inabaki na haki ya kuonyesha kazi zilizokamilika kwenye portfolio yake isipokuwa mteja aombe vinginevyo kwa maandishi. Kwa kazi za IT Support, jina la mteja halitajwi bila ridhaa yake.

Ownership of the final work (design, website or content) transfers to the client on full payment. DamyGaso Tech Solutions retains the right to showcase completed work in its portfolio unless the client requests otherwise in writing. For IT Support work, the client is not named without their consent.

11. Kufuta Mradi11. Cancellation

Mteja akifuta mradi baada ya kazi kuanza, malipo ya awali hayarudishwi kwa kuwa yanafidia muda na rasilimali zilizokwisha tumika.

If a client cancels a project after work has started, the deposit is non-refundable as it covers time and resources already committed.

12. Kikomo cha Dhima12. Limitation of Liability

Kampuni haitawajibika kwa hasara zisizo za moja kwa moja zinazotokana na matumizi ya mifumo, tovuti au huduma tulizotoa, ikiwemo matatizo yanayosababishwa na huduma za wahusika wengine (mfano: hosting providers, mitandao ya malipo, makampuni ya usafirishaji).

The company is not liable for indirect losses arising from the use of the systems, websites or services we provide, including issues caused by third-party services (e.g. hosting providers, payment networks, carriers).

13. Mabadiliko ya Masharti13. Changes to These Terms

Tunaweza kusasisha masharti haya mara kwa mara. Toleo la sasa litakuwa kwenye ukurasa huu.

We may update these terms from time to time. The current version will always be on this page.

14. Sheria Zinazotumika14. Governing Law

Masharti haya yanaongozwa na sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

These terms are governed by the laws of the United Republic of Tanzania.

15. Wasiliana Nasi15. Contact Us

Kwa maswali kuhusu masharti haya: DamyGaso Tech Solutions Limited, Dar es Salaam · +255 743 322 107 · [email protected] au ukurasa wa mawasiliano.

For questions about these terms: DamyGaso Tech Solutions Limited, Dar es Salaam · +255 743 322 107 · [email protected] or the contact page.